Mkuu wa Shirika la Mwezi Mwekundu la Palestina amesema Ijumaa kwamba hospitali nne katika eneo la kaskazini mwa Ukanda wa Gaza zimeshambuliwa katika kipindi cha saa 24, akiishutumu Israel kwa kuwalenga kwa makusudi katika jaribio la kuwalazimisha raia wa Palestina kuondoka Gaza.
“Sekta ya afya Gaza inashambuliwa”, Marwan Jilani, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Mwezi Mwekundu la Palestina ameuambia mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika mkutano kwa njia ya video. Alisema hospitali hizo Al-Shifa, Al-Awda, Al-Quds na Hospitali ya Indonesia, zote zimeshambuliwa.
Katika hospitali ya Al-Quds iliyopo Gaza City alisema mtu mmoja alifariki na wengine 20 walijeruhiwa. Mbali na kuhudumia wagonjwa, hospitali hizo zimekuwa ni makazi kwa maelfu ya wakaazi wa Gaza wanaotafuta usalama.
Forum