Mapigano ya ardhini na mashambulizi ya anga yaliendelea usiku kucha huko Gaza. Hospitali ya Shifa ambayo ni kubwa sana huko Gaza imezingirwa kabisa, mkurugenzi wake Mohammad Abu Salmiya, alisema Jumamosi jioni.
Jeshi la Israel lilisema jumamosi litasaidia kuwahamisha watoto wachanga leo Jumapili kutoka hospitali ya Shifa ambako kuna mzozo mkubwa sana wa kibinadamu. “Tutatoa msaada unaohitajika”, msemaji mkuu wa jeshi la Israel, Admirali Daniel Hagari alisema Jumamosi.
Watoto wawili walifariki Jumamosi huko Shifa na wengine kadhaa wako hatarini wakati mafuta ya kuendesha jenereta yanakwisha. “Vifaa vya matibabu havifanyi kazi.
Wagonjwa hasa wale walio katika chumba cha wagonjwa mahututi, walianza kufa”, Mkurugenzi wa Hospitali ya Shifa Mohammed Abu Selmia alisema kwa njia ya simu huku milio ya risasi na milipuko ilisikika nyuma yake.
Forum