Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 15:07

Rais Biden kusikiliza maoni ya Waislamu kuhusu vita vya Israel na Hamas


Rais wa Marekani Joe Biden (Kulia) na Rais wa Indonesia Joko Widodo (kushoto) wakiwa Hiroshima Mei 20, 2023. Picha na Kitini / Wizara ya Mambo ya Nje ya Japani / AFP.
Rais wa Marekani Joe Biden (Kulia) na Rais wa Indonesia Joko Widodo (kushoto) wakiwa Hiroshima Mei 20, 2023. Picha na Kitini / Wizara ya Mambo ya Nje ya Japani / AFP.

Rais wa Marekani Joe Biden anatazamiwa kusikiliza maoni ya jumuiya za Kiislamu kuhusu vita vya Gaza wakati wa mkutano na Rais wa Indonesia Joko Widodo katika Ikulu ya Marekani Jumatatu mchana.

Widodo yuko Washington ili kuinua uhusiano wa kidiplomasia naz "ushirikiano wa kimkakati wa kina," wa juu kabisa katika nafasi ya kidiplomasia ya nchi hiyo.

Viongozi hao wenye tofauti kubwa ya maoni kuhusu mzozo huo, wakati Biden akiiunga mkono Israel bila ya kutetereka, na Widodo akitaka kusitishwa mara moja kwa mapigano huko Gaza na kuunga mkono tume ya Umoja wa Mataifa ambayo imekuwa ikikusanya ushahidi wa uhalifu wa vita unaodaiwa kufanywa na pande zote mbili tangu shambulizi la Hamas la Oktoba 7.

Widodo atakutana na Biden kufuatia mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu, au OIC, uliofanyika Riyadh, Saudi Arabia mwishoni mwa wiki. Mkutano huo uliyakutanisha mataifa 57 yenye Waislamu wengi ikiwemo Jumuiya ya kiarabu.

Tamko lake lilikataa uhalali wa Israeli kwa vitendo vyake huko Gaza kama kujilinda na kutaka kumalizwa mara moja kwa vita.

Mkutano huo ulitoa wito wa kusitishwa kwa uuzaji wa silaha kwa Israel na kuongeza upatikanaji wa misaada ya kibinadamu.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kutoka Washington Jumapili jioni, Widodo alisema kwamba atafikisha maazimio ya mkutano huo kwa Biden. "Israel lazima iwajibike kwa ukatili inaoufanya," alisema.

Indonesia siyo muhusika wa kikanda kama Misri, Jordan au Qatar yenye majukumu muhimu katika mipango ya haraka ya utawala, kama vile kuhakikisha kuachiliwa kwa mateka na kuanzisha njia za kibinadamu katika eneo la Gaza.

Ikiwa kama nchi yenye idadi kubwa sana ya Waislamu, sauti ya Jakarta inabeba nguvu katika mipango ya utawala ya muda mfupi na mrefu ya kusuluhisha mzozo huo na kushughulikia suala hilo kuelekea njia ya amani.

Takriban Waislamu milioni 229 wanaishi Indonesia, ikiwa ni asilimia 87 ya watu . Hivyo ni asilimia 13 ya idadi ya Waislamu duniani.

Forum

XS
SM
MD
LG