Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 06:59

Seneta Tim Scott amejitoa rasmi katika kinyang'anyiro cha urais Marekani 2024


Seneta Tim Scott kutoka jimbo la South Carolina nchini Marekani.
Seneta Tim Scott kutoka jimbo la South Carolina nchini Marekani.

Seneta huyo wa jimbo la South Carolina alitoa tangazo hilo katika kituo cha Fox News Channel. Scott anasema "Nadhani wapiga kura ambao ni watu muhimu zaidi hapa duniani wamekuwa wazi wananiambia kwamba, Tim, sio hivi sasa".

Mgombea urais kupitia chama cha Republican, Tim Scott anasema anajiondoa katika ushindani wa kuwania urais mwaka 2024 ikiwa ni hatua ambayo iliwashangaza wafadhili wake na wafanyakazi wake wa kampeni.

Seneta huyo wa jimbo la South Carolina alitoa tangazo hilalitangaza hatua yake katika kituo cha Fox News Channel kwenye kipindi cha “Sunday Night in America” na Trey Gowdy. Scott anasema, Nadhani wapiga kura ambao ni watu muhimu zaidi hapa duniani wamekuwa wazi wananiambia kwamba, Tim, sio hivi sasa.

Uamuzi huo unakuja wakati Scott akiendelea kupambana katika uchaguzi katika uwanja uliotawaliwa na Rais wa zamani Donald Trump. Scott ambaye ni Mrepublican pekee mweusi katika Seneti, aliingia katika kinyang'anyiro hicho kwa fedha nyingi kuliko mgombea mwingine yeyote wa Republican lakini hakuweza kupata njia ya kujinasua.

Forum

XS
SM
MD
LG