Viongozi hao wakiongozwa na Imam mashuhuri Mahmoud Dicko wanakutana na viongozi wa kijeshi katika kambi ya kijeshi ambako uwasi ulianza wiki iliyopita na kusababisha kuondolewa madarakani kwa Rais Keita kwa mazungumzo yao ya kwanza Jumatano juu ya utaratibu wa mpito.
Viongozi wa baraza la kijeshi hawakufikia makubaliano na ujumbe wa ECOWAS mapema wiki hii juu ya kuunda utawala wa mpito wa kiraia pale wanajeshi walipoeleza kwamba suala hilo litajadiliwa kati ya raia wa Mali wenyewe.
Wakati huo huo Rais wa Senegal Macky Sal anakutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini Paris kujadili hali ya huko Mali na janga la corona.
Mapema Jumatano Maafisa wa Umoja wa Ulaya (EU) wamesema Jumuiya hiyo inasitisha kazi zake za kutoa mafunzo ya kijeshi nchini Mali kufuatia mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Rais Keita.
Afisa wa EU amesema miradi miwili ya kutowa mafunzo kwa jeshi na polisi ikiwa ni sehemu ya juhudi za kimataifa kurudisha utulivu Mali na kuimarisha utawala wa taifa imesimamishwa kwa sababu lengo lilikuwa kusaidia serikali halali ya nchi hiyo.
Afisa huyo amesema mawaziri wa ulinzi wa EU wanaokutana Berlin Jumatano, watazungumzia hali ya Mali.
Kwa upande mwengine jumuiya ya mataifa 88 yanayozungumza kifaransa OIF yamesitisha uwanachama wa Mali kutoka jumuia hiyo, kufuatana na Kaibu mkuu Louise Mushikiwabo.
OIF imetowa wito wa kuachiliwa mara moja kwa Keita na maafisa wengine wa serikali yake wanoshikiliwa na wanajeshi tangu Agosti 18.