Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 00:55

Vikosi vya usalama Uganda vyaanza kuwadhibiti wapinzani wa Museveni 


Rais Yoweri Museveni
Rais Yoweri Museveni

Vikosi vya usalama nchini Uganda vinafanya msako kwa waandishi wa habari ambao wanafuatilia na kutoa changamoto dhidi ya utawala wa miaka 34 wa Rais Yoweri Museveni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza Reuters shirika moja la uangalizi limesema operesheni hiyo inafanyika kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2021.

Nayo taasisi yenye makao yake mjini New York, Marekani ya Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ) imesema imeweka kumbukumbu ya kesi za waandishi wa habari walau 10 walioshambuliwa na wana usalama, kuwekwa kizuizini, au kushtakiwa kwa makosa yanayo husiana na kufanya kazi zao mwaka huu, ikilinganishwa na kesi nne kama hizo mwaka jana.

Polisi na jeshi wamegeuza ripoti za kisiasa kuwa kazi hatari, alisema Muthoki Mumo, mwakilishi wa taaisisi hiyo ya Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Fred Enanga, waziri wa habari Judith Nabakooba na msemaji wa rais, Don Wanyama, walitafutwa kwa simu lakini hawakujibu.


XS
SM
MD
LG