Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:46

Uganda yawaachia huru wafungwa zaidi raia wa Rwanda


Rais wa Uganda Yoweri Museveni na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame.

Serikali ya Uganda Jumanne ilifichua kwamba inawazuilia raia 39 wa Rwanda baada ya kuachilia wengine zaidi 13 na kufikisha idadi ya raia wa Rwanda walioachiliwa na Uganda kuwa 22. 

Waziri wa mambo ya nje wa Uganda Sam Kutesa, alisema wanaozuiliwa katika magereza ya nchi hiyo wanatumikia vifungo mbalimbali.

Kutesa alikanusha madai ya serikali ya Rwanda kwamba Uganda inawazuiliwa raia wake bila makosa, akisisitiza kwamba wanaozuiliwa wamepatikana na makosa ya kuhatarisha usalama wa Uganda.

Katika hafla ya kuachiliwa raia hao wa Rwanda, iliyofanyika jumanne jijini Kampala, Kutesa alisema hakuna mtu amekamatwa Uganda kutoka Rwanda eti tu kwa sababu ni raia wa Rwanda.

“Hawakamatwi kwa sababu ni raia wa Rwanda, na nataka hilo lieleweke. Watu hawa walikamatwa kwa sababu walifanya uhalifu wakiwa na lengo la kuhatarisha usalama wa Uganda na yeyote anayefanya makosa kama hayo, atakamatwa,” amesema Kutesa.

Waziri huyo alisema Uganda inataka Rwanda nayo kuachilia huru raia wake wanaozuiliwa katika maagereza yake.

“Tulikuwa na mkutano mjini Kigali na walisema walikuwa tayari wameachiliwa watu wetu wawili. Kwa upande wetu, tunafanya kile ambacho ni muhimu katika kurejesha uhusiano mwema. Hii si ishara kwamba watu hawa hawana hatia,” aliendelea kusema.

Tuhuma dhidi ya washukiwa

Kutesa alisema kati ya walioachiliwa kufikia sasa wamejihusisha katika kufanyia ujasusi serikali ya Rwanda na makosa mengine yanayohusiana na usalama mwaka 2019.

Miongoni mwao walikuwa wamefunguliwa kmashtaka katika mahakama ya kijeshi kwa makosa ya kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Uganda iliachilia huru raia 9 wa Rwanda Januari 8 2020.

Rwanda inadai kwamba zaidi ya raia wake 100 wanazuiliwa Uganda kinyume cha sheria na kutaka wote waachiliwe huru.

Viongozi kukutana mpakani

Rais wa Uganda Yoweri Museveni na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame, wanatarajiwa kukutana kwenye mpaka wa nchi hizo wa Gatuna, ambao umefungwa tangu mwaka uliopita, Ijumaa wiki hii tarehe 21 Februari 2020 katika hatua ambayo wachambuzi wanasema itakuwa fursa nzuri ya kufungua mpaka huo.

Kulingana na mwandishi wa sauti ya Amerika mjini Kigali, matayarisho ya mkutano huo yanaendelea vizuri lakini mpangilio maalum kuhusu yatakayofanyika wala kujadiliwa haujatolewa.

Mwandishi wetu hata hivyo amesema inatarajiwa kwamba marais Joao Lourenco wa Angola na Felix Tshisekedi, watahudhuria mkutano huo wa ijumaa.

Kauli za viongozi wa Uganda na Rwanda

Jumapili, rais wa Rwanda Paul Kagame, alisisitiza kwamba hatasurutishwa kufungua mpaka huo hadi pale Uganda itakapotimiza matakwa ya Rwanda.

Serikali ya Uganda inasema hatua ya kufunga mpaka huo inaweka doa ushirikiano wa jumuiya ya Afrika mashariki na kwamba hakuna anayefaidhika na hatua hiyo kando na kila upande kupata hasara ya kibiasahra na kueneza uhusiano mbaya.

Kamati maalum iliyoundwa kusimamia mazungumzo kati ya Rwanda na Uganda inaripotiwa kupendekeza katika kikao cha ijumaa wiki iliyopita mjini Kigali, kwamba viongozi hao wafungue mpaka watakapokutana ijumaa wiki hii.

Kamati hiyo vile vile ilitaka pande husika kuheshimu haki za kibinadamu kwa raia wa pande zote.

Rwanda inadai kwamba Uganda inaunga mkono makundi ya waasi yenye lengo la kupindua serikali ya rais Paul Kagame, huku utawala wa rais wa Uganda Yoweri Museveni ukidai kwamba Rwanda inapanga kutatiza usalama wa Uganda.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Kennes Bwire, VOA, Washington DC.

XS
SM
MD
LG