Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 00:56

Vikosi vya RSF vyadai kuliteka jiji la Nyala Sudan


Picha ya iliyochukuliwa kutoka katika mtandao wa X ikimuonyesha kamanda RSP Mohamed Hamdan Daglo akiwahutubia wapiganaji wa RSF katika eneo lisilojulikana.
Picha na Vikosi vya RSF/ AFP
Picha ya iliyochukuliwa kutoka katika mtandao wa X ikimuonyesha kamanda RSP Mohamed Hamdan Daglo akiwahutubia wapiganaji wa RSF katika eneo lisilojulikana. Picha na Vikosi vya RSF/ AFP

Vikosi vya kijeshi vya Msaada wa Dharura (RSF) ambavyo vimekuwa vikipambana na jeshi la Sudan kwa ajili ya udhibiti nchi hiyo vimesema vimeliteka jiji la pili kwa ukubwa la Nyala siku ya Alhamisi.

Kutekwa kwa mji mkuu huo wa jimbo la Darfur Kusini lililopo Magharibi mwa nchi inaweza kuashiria hatua ya mabadiliko katika miezi sita ya vita vya Sudan, na yamekuja wakati pande hizo mbili zinapaswa kuanza tena mazungumzo huko Jeddah.

Jeshi halikujibu ombi la kutoa maoni, na kukatika kwa mtandao kulifanya iwe vigumu kuthibitisha dai hilo mara moja.

Wakati RSF limetawala sehemu kubwa ya ardhi ya mji mkuu wa Khartoum, jeshi limeweza kulinda kambi zake muhimu zilizoko katika mji huo.

Wakati huo huo sehemu kubwa ya serikali imehamia katika Bandari ya Sudan kwenye pwani ya Bahari ya Shamu.

RSF ilisema katika taarifa kwamba wamekamata makao makuu ya jeshi huko Nyala na kuchukua vifaa vyake vyote.

Picha kutoka kwenye video ya UGC iliyotumwa kwenye jukwaa la X Agosti 22, 2023 imeripotiwa ikiwaonyesha wanajeshi wa Sudan wakiwafyatulia risasi wapiganaji RSF huko Khartoum. Picha na UGC / AFP
Picha kutoka kwenye video ya UGC iliyotumwa kwenye jukwaa la X Agosti 22, 2023 imeripotiwa ikiwaonyesha wanajeshi wa Sudan wakiwafyatulia risasi wapiganaji RSF huko Khartoum. Picha na UGC / AFP

Ilichapisha kanda ya video, ambayo shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha, wakionyesha wanajeshi wake wakishangilia kwa milio ya risasi, wakidai kuwa wameiteka ngome.

Pia ilichapisha video ya kamanda wa pili wa RSF Abdelrahim Dagalo, ambaye amewekewa vikwazo na Marekani, na kusema alikuwa akiongoza juhudi hizo.

Nyala, ni kituo cha biashara ambacho waangalizi wanasema kinaweza kutumika kama ngome ya RSF, limekuwa eneo la mapigano makali, ambapo mashambulizi ya anga na mizinga limeua watu wengi, kuharibu makazi ya raia, kulemaza huduma za msingi.

RSF pia imechukua udhibiti wa Zalingei, mji mkuu wa jimbo la Kati la Darfur.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG