Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:20

Vifo vya watoto kutokana na bunduki Marekani vyafikia kiwango cha juu zaidi


Waandamanaji mjini Nashville,Tennessee wakitetea usalama shuleni.
Waandamanaji mjini Nashville,Tennessee wakitetea usalama shuleni.

Vifo vya watoto vinavyotokana na bunduki nchini Marekani vimefikia kiwango cha juu zaidi, kulingana na utafiti mpya uliochapishwa na Chuo cha Marekani cha Madaktari wa Watoto.

Kwa kutumia takwimu ya Vifo kutoka kwa taasisi ya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, utafiti uliochapishwa Jumatatu katika jarida la AAP Pediatrics, ulibainisha kuwa watoto 4,752 walikufa kutokana na majeraha yanayohusiana na bunduki mnamo mwaka wa 2021, ambao ambazo ndizo takwimu za hivi karibuni kabisa, kutoka 4,368 mnamo mwaka wa 2020 na 3,390, mwaka 2019.

Vurugu zinazohusishwa na bunduki zimekuwa sababu namba 1 ya vifo vya watoto nchini Marekani tangu mwaka 2020.

Utafiti huo ulichapishwa huku wabunge wa jimbo la Tennessee wakifungua kikao maalum kuhusu usalama wa umma, baada ya shambulizi la risasi katika shule ya Nashville mapema mwaka huu, lililowaua watoto watatu na walimu watatu. Annie Andrews, daktari wa watoto wa Carolina Kusini na mtafiti wa kuzuia mashambulizi ya kutumia bunduki, ambaye hakuhusika katika uchunguzi huo, alisema kwamba alipokuwa daktari, “hakudhani kamwe kwamba angetunza watoto wengi hivyo, wenye majeraha ya risasi.

"Lakini ukweli wa mambo ni kwamba, katika kila hospitali ya watoto kote nchini, kuna watoto katika vyumba vya wagonjwa mahututi wanaouguza majeraha ya bunduki, " alisema Andrews

Utafiti huo ulionyesha kwamba asili mia 67 ya watoto waliouawa na bunduki, ni weusi huku asili mia 78% ya watu wanaojiua kwa kutumia bunduki wakiwa ni watoto wazungu.

Forum

XS
SM
MD
LG