Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 06:49

Wachambuzi wasema Russia na China zinadhani upanuzi wa BRICS ni ushindi wa kimaadili


Muonekano wa ukumbi wa mikutano wa Sandton, mahala utakapofanyika mkutano wa BRICS huko Johannesburg Afrika Kusini. Picha na REUTERS/James Oatway
Muonekano wa ukumbi wa mikutano wa Sandton, mahala utakapofanyika mkutano wa BRICS huko Johannesburg Afrika Kusini. Picha na REUTERS/James Oatway

Russia na China zinatazamia kuongeza ushawishi wao wa kisiasa na kiuchumi wakati wa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya nchi zinazoendelea haraka kiuchumi BRICS utakaofanyika Afrika Kusini wiki hii.

Nchi hizo zinatarajiwa kwa pamoja pia, kuongeza malalamiko yao dhidi ya nchi za Magharibi pale zitakapochukua hatua kubwa na rasmi ya kuileta Saudia Arabia karibu zaidi.

Viongozi wa Jumuiya ya kiuchumi ya BRICS ambazo ni Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini watakuwa na mkutano wa siku tatu katika wilaya ya kifedha ya Sandton, jijini Johannesburg utahudhuriwa na rais wa China Xi Jinping ambaye atasisitiza juu ya mtaji wa kidiplomasia ambao nchi yake imewekeza katika umoja huo mnamo kipindi cha zaidi ya muongo mmoja na imekuwa ni njia nzuri kwa malengo yake.

Rais wa Russia Vladimir Putin atahudhuria mkutano huo kwa njia ya mtandao, kutokana na hati ya kumkamata iliyotolewa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu, endapo atasafiri kwenda Afrika Kusini, kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine.

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa watakuwepo kwenye mkutano huo pamoja na rais wa China.

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na mkewe Rosangela da Silva walipowasili Afrika ya Kusini Agosti 21 2023.
Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na mkewe Rosangela da Silva walipowasili Afrika ya Kusini Agosti 21 2023.

Mkutano mkuu wa kilele utakaofanyika siku ya Jumatano - na mikutano ya pembeni itafanyika siku ya Jumanne na Alhamisi - unatarajiwa kutoa wito jumla wa kutaka ushirikiano zaidi kati ya nchi za Ukanda wa Kusini ya dunia, huku kukiwa na ongezeko la hali ya kutoridhika kwao na dhana kwamba nchi za magharibi zina ushawishi mkubwa zaidi kwenye taasisi za kimataifa.

Hiyo ndiyo dhana ambayo Russia na China zinafurahia kuegemea. Viongozi au dazeni ya wawakilishi kutoka nchi zinazoendelea wanatarajiwa kuhudhuria mikutano ya pembeni itakayofanyika katika jiji hilo tajiri kuliko yote barani Afrika ili kuwapatia Xi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov, idadi kubwa zaidi ya wajumbe.

Hilo likiwa ni moja wapo ya suala muhimu la kisiasa litakalojadiliwa na pengine uwamuzi kuchukuliwa kuhusu kuongeza idadi ya wajumbe kwenye jumuiya hiyo ya BRICS, ambayo iliundwa mwaka 2009 na nchi zinazokuwa haraka kuichumi za Brazil, Russia, India na China, na kuiongeza Afrika Kusini mwaka uliofuata.

Rais wa Russia Vladimir Putin akipeana mkono na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa huko Saint Petersburg, Russia, June 17, 2023.. Picha na REUTERS
Rais wa Russia Vladimir Putin akipeana mkono na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa huko Saint Petersburg, Russia, June 17, 2023.. Picha na REUTERS

Saudi Arabia ni moja kati ya nchi zaidi ya nchi 20 zilizotuma maombi rasmi ya kujiunga na BRICS katika uwezekano wa upanuzi, wanasema maafisa wa Afrika Kusini.

Hatua yoyote ya kujumuishwa kwa mzalishaji mkuu wa pili wa mafuta duniani katika kundi la kiuchumi iliyopo Russia na Uchina ni wazi itatupiwa jicho na Marekani na washirika wake katika hali isiyo nzuri ya kisiasa dunaini, na hasa kufuatia hatua ya hivi karibuni ya Beijing kutumia ushawishi wake katika Ghuba ya Uajemi.

Wachambuzi wanasema, hata ikiwa kutakuwa na makubaliano kuhusu msingi wa kupanua BRICS, ambayo tayari ina inaleta pamoja sehemu kubwa ya nchi zenye uchumi mkubwa katika nchi zinazoendelea duniani, huo ni ushindi wa kimaadili kwa malengo ya Russia na Uchina kuifanya jumuiya hiyo kuwa wizani sawa na kundi la mataifa tajiri la G-7.

Pande zote mbili zinapendelea kuongezwa kwa nchi zaidi ili kuimarisha aina fulani ya muungano, katikati ya mvutano wa kiuchumi kati ya Uchina na Marekani na sawa na aina ya vita baridi vya Russia na nchi za Magharibi kwa sababu ya vita nchini Ukraine.

Mataifa kuanzia Argentina hadi Algeria, Misri, Iran, Indonesia na Umoja wa Falme za Kiarabu zimeomba rasmi kujiunga pamoja na Saudi Arabia, na pia inawezekana kuwepo na wanachama wengine wapya.

Forum

XS
SM
MD
LG