Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 21:31

Afrika kusini itakuwa mwenyeji wa BRICS wiki ijayo


Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa akizungumza katika moja ya mikutano ya BRICS Business. Nov. 13, 2019.
Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa akizungumza katika moja ya mikutano ya BRICS Business. Nov. 13, 2019.

Mkutano wa BRICS wiki ijayo utatupiwa jicho zaidi kuhusu  uhusiano kati ya Pretoria na Kremlin ambao wengine ni habari njema na kwa baadhi ni jambo la kushangaza. Moscow na chama cha ANC zilijenga uhusiano wakati wa vita baridi

Afrika Kusini itakuwa mwenyeji wa mkutano wa BRICS wiki ijayo ambao utatupiwa jicho zaidi kuhusu uhusiano kati ya Pretoria na Kremlin ambao wengine ni habari njema na kwa baadhi ni jambo la kushangaza.

Moscow na chama cha African National Congress cha Afrika Kusini zilijenga uhusiano wakati wa vita baridi, wakati Umoja wa Sovieti ulipounga mkono vita vya ANC dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Uhusiano huo unabaki kuwa imara licha ya mabadiliko ya kihistoria na kiitikadi ambayo kimantiki yangeweza kusababisha mgawanyiko muda mrefu uliopita.

Mwaka 1991, Umoja wa Sovieti ulivunjika, na kupanda mbegu za utaifa kwa mwanachama muhimu, Russia chini ya Vladimir Putin. Nchini Afrika Kusini hata hivyo ushindi dhidi ya ubaguzi wa rangi ulileta demokrasia na katiba ya kiliberali zaidi barani Afrika ikikishinda chama cha ANC kwa taswira ya ulimwengu kama mkombozi

Forum

XS
SM
MD
LG