Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:00

Biden kuhudhuria mkutano wa G20 nchini India


Biden Modi
Biden Modi

Rais wa Marekani Joe Biden atahudhuria Mkutano wa mataifa yenye nguvu za kiuchumi duniani, G20, mjini New Delhi, India, lakini hataudhuria Mkutano wa Marekani na Jumuiya ya ASEAN, na Asia Mashariki huko Jakarta, Indonesia.

Badala yake atawakilishwa na Makamu wa Rais Kamala Harris, White House ilitangaza Jumanne.

Katika kile kinachotajwa kama uthibitisho wa umuhimu ambao Biden anaipatia serikali ya Waziri Mkuu Narendra Modi, rais huyo atakuwa India kuanzia tarehe 7-10, mwezi Septemba mwaka huu, akiwasili siku mbili kabla ya mkutano huo wa kila mwaka, wa viongozi wa nchi hizo 20.

Wakuu wa nchi na serikali wamepangiwa kuanza mikutano yao tarehe tisa na kumi mwezi Septemba, wakitarajiwa kujadili masuala ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na mikakati ya kwelekea kwa nishati safi, kupunguza athari za kiuchumi na kijamii, za vita vya Ukraine, na kuongeza uwezo wa benki za maendeleo za kimataifa.

White House isema kwamba akiwa New Delhi, Biden atathibitisha kujitolea kwa Marekani kwa G20, kama jukwaa kuu la ushirikiano wa kiuchumi, pamoja na nchi yake kuwa mwenyeji wa mkutano huo hapo mwaka wa 2026.

Kwa mujibu wa mshauri wa usalama wa kitaifa wa Marekani, Jake Sullivan Mkutano wa Marekani na nchi za ASEAN unahitimisha mikutano rasmi ya ngazi ya juu kati ya Marekani na Muungano wa Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN) ambayo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alishiriki mwezi uliopita.

Mkutano wa wakuu wa Asia Mashariki ni kongamano la kikanda linalofanyika kila mwaka na ASEAN, na washirika wake ni pamoja na Marekani, China na Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG