Zaidi ya watu 110 wamefariki kutokana na moto huo, idadi ambayo inatarajiwa kuongezeka siku zijazo.
Idadi ya watu waliopotea bado haijulikani, lakini vikosi vya wizara ya Ulinzi ya Marekani vimetumwa kusaidiana na waokoaji waliofika katika eneo hilo awali.
Maafisa wa jeshi la ardhini la Marekani na Walinzi wa Kitaifa walijiunga na timu za utafutaji na uokoaji, na mamlaka ya Usimamizi wa Dharura ya serikali kuu, au FEMA, inasema juhudi za kutoa msaada zimefanikiwa kufikia sasa.
"Kwa sasa, juhudi za utafutaji zimefanyika kwa kiasi cha asili mia 78% katika mji wa Lahaina. Na tunaendelea kuwa na timu zetu kukagua mifumo yote ambayo iliyoathiriwa na moto huu,’ alisema mkuu wa FEMA, Diane Criswell.
Alisema FEMA tayari imetoa zaidi ya $8 milioni kwa familia ambazo zimeathiriwa, na kwamba idadi ya watu waliokuwa kwenye makazi ya muda imepungua haditakriban 40 na ni zaidi ya watu 1,200 ambao wamehamishwa hadi kwenye hoteli, na aina zingine za nyumba za kukodishwa kwa muda.
Forum