Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 08:43

Trump na washirika wake 18 wana kesi za kujibu 41 katika jimbo la Georgia


Aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump Aug. 4, 2023
Aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump Aug. 4, 2023

Aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump na washirika wake 18, wamepatikana na mashtaka ya kujibu katika jaribio lao la kutaka kubatilisha matokeo ya uchaguzi mkuu mwaka 2020, katika jimbo la Georgia.

Trump na washirika wake wanashutumiwa kwa kujaribu kuvuruga matokeo ya uchaguzi katika jimbo la Georgia ambalo alishindwa na rais Joe Biden.

Anadaiwa kumshurutisha msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo, mrepublican, kutafuta kura za kutosha kumpa ushindi ili aendelee kusalia madarakani.

Anashutumiwa pia kuendelea kusema madai ya uongo kwamba uchaguzi mkuu ulikumbwa na udanganyifu na kujaribu kushawishi wabunge wa jimbo la Georgia kutotilia maanani maamuzi ya wapiga kura na kuchagua waidhinishaji feki wa uchaguzi kuidhinisha kwamba Trump alishinda uchaguzi huo kinyume cha sheria.

Mashtaka hayo yanaelezea namna Trump alijaribu kuvuruga mashine za kupiga kura katika jimbo la Georgia.

Wengine walioshitakiwa pamoja na Trump ni pamoja na Mark Meadows, wakili wa Trump Rudy Giuliani, aliyekuwa mwanasheria katika wizara ya sheria wakati wa Trump Jeffrey Clark ambaye alikuwa msitari wa mbele katika kutaka kubatilisha matokeo ya uchaguzi katika jimbo la Georgia.

Mawakili waliokuwa wakimshauri Trump wakiwemo John Eastman, Sidney Powell na Kenneth Chesebro pia wamepatikana na makosa ya kujibu.

Wote walioshitakiwa wataruhusiwa kujiwasilisha mahakamani adhuhuri Augosti 25.

Waendesha mashtaka wanapanga kuanza kesi hiyo katika muda wa miezi sita kuanzia leo.

Forum

XS
SM
MD
LG