Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 07:10

Vatican: Muumini asafiri kutoka Venice kuuaga mwili wa hayati Benedict

Mwiii wa hayati Benedict ukiwa katika kanisa la St. Peter, Vatican.
Mwiii wa hayati Benedict ukiwa katika kanisa la St. Peter, Vatican.

Fillipo Tuccio, mwenye umri wa miaka 35, ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba  alikuwa amesafiri  usiku kucha  kwa treni kutoka Venice kuja kuuona mwili wa Benedict.

Waumini wanajipanga mistari katika Kanisa la St. Peter Jumatatu kutoa heshima zao za mwisho kwa Papa Benedict ambaye mwili wake umewekwa katika eneo hilo.

Baadhi ya watu walikuwa wanasubiri kwa saa kadhaa hadi milango ilipofunguliwa.

Papa mstaafu huyo alifariki Jumamosi asubuhi akiwa na umri wa miaka 95. Benedict alikuwa ni papa wa kwanza katika miaka 600 kustaafu kutoka wadhifa wake huo.

Fillipo Tuccio, mwenye umri wa miaka 35, ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba alikuwa amesafiri usiku kucha kwa treni kutoka Venice kuja kuuona mwili wa Benedict.

“Alikuwa mtu muhimu sana kwangu: kwa vile nilivyo, njia yangu ya kufikiri, maadili yangu. Ndiyo maana nilitaka kuja kutoa heshima za mwisho leo,” Tuccio alisema.

Mwili wa Benedict, ambao umevalishwa nguo nyekundu ya kitamaduni, utaendelea kuwepo kwa ajili ya kuagwa na umma hadi Jumatano.

Papa Francis akiwa na Papa mstaafu Benedict, March 23, 2013. REUTERS/Osservatore Romano/File Photo
Papa Francis akiwa na Papa mstaafu Benedict, March 23, 2013. REUTERS/Osservatore Romano/File Photo

Siku ya Alhamisi, “Papa Francis atakuwa mtu wa kwanza katika historia ya zama zetu kuongoza kama Papa katika mazishi ya mtangulizi wake,” kulingana na tovuti ya habari ya Vatican.

“Mungu, nakupenda,” inaelezwa yalikuwa maneno ya mwisho ya Benedict aliyotamka muda mchache kabla ya kufariki, habari za Vatican zilieleza.

Baadhi ya taarifa hizi zinatokana na shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG