Papa Benedict alifariki Jumamosi akiwa na umri wa miaka 95, na atakumbukwa kama kiongozi wa kwanza wa kanisa katoliki katika historia ya miaka 600 kujiuzulu kutoka wadhifa wake. Filippo Tucccio mwenye umri wa miaka 35 na ambaye ni mkazi wa mji wa Venice Italy amesema kwamba alisafiri usiku kucha kwa treni, ili kupata nafasi ya kuutazama mwili huo.
Mwili wa Benedict ukiwa umevishwa magwanda ya kitamaduni na utalazwa kwenye kanisa hilo hadi Jumatano. Siku ya Alhamisi, Papa Francis atakuwa kiongozi wa kwanza wa kanisa kitoliki katika miaka ya karibuni kuongoza mazishi ya mtangulizi wake, kulingana na mtandao wa habari wa Vatican. ”Mungu wangu nakupenda”, ndiyo maneno ya mwisho aliyosema kabla ya kukata roho kulingana na chombo cha habari cha Vatican