Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 21:30

Papa Francis aadhimisha siku ya amani duniani kwa utamaduni wa kanisa Katoliki


Pope Francis aliposherehekea misa ya mkesha wa Krismasi katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, tarehe 24 Desemba 2022. REUTERS
Pope Francis aliposherehekea misa ya mkesha wa Krismasi katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, tarehe 24 Desemba 2022. REUTERS

Papa Francis aliadhimisha Siku ya Amani duniani kwa utamaduni wa kanisa Katoliki siku ya Jumapili lakini mwanzo wa mwaka mpya huko Vatican uligubikwa na kifo cha mtangulizi wake, Benedict.

Francis aliongoza Misa katika Kanisa la Mtakatifu Petro huku mwili wa Benedict, aliyefariki Jumamosi akiwa na umri wa miaka 95, ukitayarishwa kwa siku tatu za watu kutoa heshima zao katika kanisa hilo kuanzia Jumatatu.

Kwa mujibu wa matakwa ya Benedict, mazishi yake siku ya Alhamisi yatakuwa ya kawaida, ya ukimya na ya kiasi. Itakuwa mara ya kwanza katika karne nyingi kwamba papa aliyeketi madarakani ataongoza mazishi ya mtangulizi wake. Benedict, ambaye alijiuzulu mwaka 2013, alikuwa papa wa kwanza katika kipindi cha miaka 600 kujiuzulu.

Januari mosi pia ni sikukuu ya Mama Maria na katika mahubiri yake, Francis alimwomba Mama Maria kuandamana na "mpendwa wetu" Papa Mstaafu Benedict katika safari yake kutoka ulimwengu huu kwenda kwa Mungu.

Benedict pia alikumbukwa katika moja ya sala katika Misa hiyo.

XS
SM
MD
LG