Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 26, 2025 Local time: 10:06

Uturuki na Iran zataka uitishwe mkutano wa kikanda kuepusha kusambaa vita Mashariki ya Kati


Picha kwa hisani ya wizara ya mambo ya nje ya Iran, November 1, 2023, ikionyesha Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian (kushoto) akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Turkish Hakan Fidan mjini Ankara.
Picha kwa hisani ya wizara ya mambo ya nje ya Iran, November 1, 2023, ikionyesha Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian (kushoto) akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Turkish Hakan Fidan mjini Ankara.

Uturuki na Iran Jumatano zimetaka uitishwe mkutano wa kikanda wenye lengo la kuepusha kusambaa kwa vita vya Israel na Hamas.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan alikutana na mwenzake wa Iran Hossein Amirabdollahian siku moja baada ya mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Iran kukutana na viongozi wa Hamas nchini Qatar.

Iran imeonya kuwa vikundi venye silaha inavyo viunga mkono katika kanda vinaweza kuishambulia Israel kutokana na vita vyake kwa Hamas.

Fidan alisema Uturuki ilikuwa inashinikiza sitisho la haraka la vita kwa sababu “siyo vigumu kutabiri kuwa ghasia hizi zinaweza kukua” bila ya kuwepo suluhisho la kudumu la vita.

“Hatutaki janga la kibinadamu huko Gaza kugeuka kuwa vita vitakayo athiri nchi za kanda hiyo,” Fidan alisema.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran “alituarifu kuwa kuna dalili zenye nguvu kuna uwezekano wa vikundi venye silaha katika kanda hiyo kuingilia katika vita hivyo iwapo hali haitabadilika,” Fidan alisema. “Sitisho la mapigano na amani ni mambo ambayo yamekuwa muhimu sana.”

Amirabdollahian alisema mkutano wa amani utazihusisha nchi za “Kiislam na Kiarabu” ni lazima ufanyike “haraka iwezekanavyo.”

Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan (kushoto) akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amirabdollahian mjini Ankara, Uturuki.
Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan (kushoto) akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amirabdollahian mjini Ankara, Uturuki.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran baadaye alikutana na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan mjini Ankara.

Israel imekuwa ikishambulia Ukanda wa Gaza tangu wananchama wa Hamas waliokuwa na silaha walipovuka mpaka Oktoba 7 na kuua zaidi ya watu 1,400, wengi wao raia kulingana na maafisa wa Israeli.

Kampeni ya mashambulizi hayo imesababisha vifo vya zaidi ya watu 8,796, theluthi mbili yao ni wanawake na watoto, kulingana na wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG