Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 17, 2024 Local time: 20:36

Hasira zaongezeka Iran kufuatia kukamatwa kwa wakili wa kutetea haki za binadamu


Maandamano ya kuitisha haki zaa binadamu ya Iran. Picha ya maktaba.
Maandamano ya kuitisha haki zaa binadamu ya Iran. Picha ya maktaba.

Kukamatwa kwa wakili wa haki za binadamu wa Iran aliyewahi kuwa mshindi wa tuzo, kumeongeza hasira miongoni mwa makundi ya haki za binadamu, kufuatia kifo cha msichana mdogo ambaye wanaharakati wamesema alipigwa vibaya na polisi wa maadili wa Tehran.

Nasrin Sotoudeh mwenye umri wa miaka 60 alikamatwa Jumapili kwenye mazishi ya msichana Armita Garawand mwenye umri wa miaka 17, ambaye kifo chake kilitangazwa na chombo cha habari cha serikali, baada ya kupoteza fahamu kwa mwezi mmoja.

Tukio hilo lililofanyika Oktoba mosi limeibua kisa cha Mahsa Amini msichana aliyekufa akiwa mikononi mwa polisi Septemba mwaka jana, baada ya kuzuiliwa kwa madai ya kutovaa hijabu, wakati mamlaka zikijitahidi kuzuia maandamano sawa na yaliyofuatia kifo chake.

Wakili Sotoudeh ambaye ndani ya muongo mmoja uliyopita amekuwa nje na ndani ya jela kufuatia kesi kadhaa kutokana na uanaharakati wake, muda mfupi baada ya kukamatwa alipelekwa kwenye jela ya wanawake ya Qarchak,iliyopo nje ya Tehran, kulingana na ujumbe wa Facebook kutoka kwa bwanake Reza Khandan.

Forum

XS
SM
MD
LG