Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 06:44

Utawala wa kijeshi Niger wataka mpango wa kuondoka majeshi ya Ufaransa


Wanajeshi wa Ufaransa wakijiandaa kwa ajili ya misheni katika kituo cha anga cha Ufaransa huko Niamey, Mei 14, 2023. Picha na ALAIN JOCARD / AFP.
Wanajeshi wa Ufaransa wakijiandaa kwa ajili ya misheni katika kituo cha anga cha Ufaransa huko Niamey, Mei 14, 2023. Picha na ALAIN JOCARD / AFP.

Viongozi wa mapinduzi ya Niger wanataka"mpango wa mashauriano" ya kuutaka utawala wa zamani wa kikoloni Ufaransa kuwaondoa wanajeshi wake, ambapo Paris inasema itakamilisha hatua hiyo mwishoni mwa mwaka.

Utawala mpya wa kijeshi umesema katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa Jumatatu jioni kwamba muda wa kuondoka "lazima uwe katika mfumo wa mashauriano na kwa makubaliano ya pande zote".

Hatua hii imekuja takriban miezi miwili tangu siku rais wa Niger Mohamed Bazoum, aliyechaguliwa kidemokrasia, alipopinduliwa tarehe 26 Julai.

Siku ya Jumapili, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitangaza kwamba Paris itamuondoa balozi wake kutoka Niger, ikifuatiwa na kikosi cha jeshi la Ufaransa katika miezi ijayo – yote ni matakwa ya utawala baada ya mapinduzi yaliyofanyika huko Niamey.

"Kuhusiana na balozi, hatuna maoni ya kutoa kuhusu mbinu za kurejea kwake," msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa Anne-Claire Legendre alisema Jumanne.

"Kuachiliwa kwa Rais Bazoum ni kipaumbele," aliongeza.

Macron, ambaye alikuwa anataka kuwa mshirika maalum wa Niger, alisema ushirikiano wa kijeshi "umekwisha" na wanajeshi wa Ufaransa wataondoka katika "miezi na wiki zijazo" watakuwa wameondoka wote "ifikapo mwisho wa mwaka".

Ufaransa ina takriban wanajeshi 1,500 katika koloni lake la zamani la Afrika Magharibi kama sehemu ya kikosi cha kupambana dhidi ya wanajihadi katika Sahel.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG