Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 23, 2024 Local time: 10:27

Viongozi wa kijeshi wa Mali, Burkina Faso na Niger watia saini makubaliano ya ulinzi

Bendera za taifa za Niger na Mali zikiwa mezani wakati wa mkutano wa ECOWAS. Picha na GERARD NARTEY / AFP.
Bendera za taifa za Niger na Mali zikiwa mezani wakati wa mkutano wa ECOWAS. Picha na GERARD NARTEY / AFP.

Mkataba wa Liptako-Gourma unaanzisha Muungano wa Nchi za Sahel (AES), kiongozi wa kijeshi wa Mali Assimi Goita alichapisha kwenye X, mtandao wa kijamii siku za nyuma   ulijulikana kama Twitter.

Viongozi wa kijeshi wa Mali, Burkina Faso na Niger siku ya Jumamosi walitia saini makubaliano ya ulinzi wa pande zote, ujumbe wa mawaziri kutoka nchi hizo tatu za Sahel ulitangaza katika mji mkuu wa Mali Bamako.

Mkataba wa Liptako-Gourma unaanzisha Muungano wa Nchi za Sahel (AES), kiongozi wa kijeshi wa Mali Assimi Goita alichapisha kwenye X, mtandao wa kijamii siku za nyuma ulijulikana kama Twitter.

Lengo ni kuanzisha muundo wa ulinzi wa pamoja na usaidizi wa pande zote kwa faida ya watu wetu", aliandika.

Eneo la Liptako-Gourma ambapo mpaka wa Mali, Burkina Faso na Niger hukutana limeharibiwa na wanajihadi katika miaka ya hivi karibuni.

Forum

XS
SM
MD
LG