Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 23, 2024 Local time: 10:33

Niger: Utawala mpya wa kijeshi wafuta hati za kusafiria za kidiplomasia


Jenerali Abdourahmane, kiongozi mpya wa Niger, apowasili kukutana na mawaziri huko Niamey, Niger Julai 28, 2023. Picha na REUTERS/Balima Boureima.
Jenerali Abdourahmane, kiongozi mpya wa Niger, apowasili kukutana na mawaziri huko Niamey, Niger Julai 28, 2023. Picha na REUTERS/Balima Boureima.

Watawala wapya wa kijeshi wa Niger wamefuta zaidi ya hati za kusafiri 990 za kidiplomasia zilizokuwa zinashikiliwa na raia wa ndani na wa kigeni wanaohusishwa na utawala ulioondolewa madarakani.

Wizara ya mambo ya nje imeandika kuwaarifu wawakilishi wa kidiplomasia nchini Niger kwamba hati zao sasa "zimepitwa na wakati", kulingana na nakala ya barua iliyobandikwa kwenye mitandao ya kijamii.

Hati za kidiplomasia zilikuwa zikishikiliwa na viongozi wakuu wa zamani katika taasisi na wizara pamoja pamoja na waliokuwa wabunge na washauri akiwemo rais na waziri mkuu, shirika rasmi la habari la ANP lilisema Alhamisi jioni.

Takriban pasipoti 50 kati ya hizo zilikuwa zimetolewa kwa raia wa Marekani, Uingereza, Ufaransa, Libya na Uturuki pamoja na nchi nyingine za Afrika Magharibi.

Rais Mohamed Bazoum alipinduliwa Julai 26 na tangu wakati huo amewekwa kwenye kizuizi cha nyumbani katika makazi yake.

Mwishoni mwa Agosti, utawala huo mpya ulifuta hati za kusafiria zilizokuwa za maafisa kadhaa wa serikali waliokuwa nje ya nchi, akiwemo waziri mkuu, waziri wa mambo ya nje na balozi wa Niger nchini Ufaransa.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG