Utawala huo uliofanya mapinduzi Julai na kumuondoa madarakani rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohamed Bazoum, mwezi uliopita, uliamuru maafisa wa Ufaransa kuondoka nchini, lakini Ufaransa haikutii amri hiyo ikisema kwamba utawala huo sio halali.
Kupitia ujumbe wa X, iliyojulikana kama Twitter, wizara hiyo imesema kwamba Stephane Jullien ambaye ni mshauri wa raia wa Ufaransa waliopo nje ya nchi alikamatwa Ijumaa iliyopita, wakati ikiitisha kuachiliwa kwake.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kwamba balozi wa Ufaransa ataendelea kubaki Niger licha ya kuombwa aondoke na utawala huo wa kijeshi. Ufaransa imekuwa ikisisitiza kwamba inatambua utawala wa Bazoum ambaye ameendelea kushikiliwa na utawala huo, huku vikwazo vikiwekewa taifa hilo na mataifa ya magharibi pamoja na mashirika ya kieneo.
Forum