Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 21:37

Biden asema kila nchi duniani ina jukumu katika kuamua hali ya baadaye ya dunia


Rais wa Marekani akihutubia Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Rais wa Marekani akihutubia Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Rais wa Marekani Joe Biden ametaka nchi zote kushirikiana katika kutatua changamoto zinazokabili dunia, akisisitiza kwamba kila nchi ina jukumu katika kuamua hali ya baadaye ya dunia.

Amesema kwamba Marekani inazingatia uwepo wa dunia ambayo kila mtu anajihisi salama, mwenye mafanikio na dunia ambayo kuna usawa.

Akihutubia kongamano la viongozi katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, hapa Marekani, Biden ameapa kuunga mkono Umoja wa Afrika na jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika magharibi ECOWAS, katika jitihada za kupinga mapinduzi ya kijeshi hasa nchini Niger na Gabon.

Amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuamua kutumwa kwa kikosi maalum cha usalama kwa ajili ya Haiti inayokumbana na makundi ya uhalifu, na kushukuru Kenya kwa kuwa mstari wa mbele katika kutaka kuisaidia Haiti.

Vile vile amesema kwamba Marekani ipo tayari kushirikiana na China katika maendeleo ya Dunia lakini haiwezi kukubali uchokozi kwa kulinda usalama na maendeleo kwa miongo kadhaa.

Biden ni rais pekee kutoka nchi wanachama wa kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa, ambaye amehudhuria kongamano hilo. Marais wa Russia, China, Ufaransa na Uingereza hawapo.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Kennes Bwire, Washington, DC

Forum

XS
SM
MD
LG