Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 18:46

Viongozi wa mapinduzi wa Niger wamshutumu mkuu wa Umoja wa Mataifa

Waziri Mkuu mteule aliyeteuliwa na utawala wa kijeshi wa wa Niger Ali Mahamane Lamine Zeine akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu Niamey, Niger Septemba 4, 2023.
Waziri Mkuu mteule aliyeteuliwa na utawala wa kijeshi wa wa Niger Ali Mahamane Lamine Zeine akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu Niamey, Niger Septemba 4, 2023.

Mashauriano  ya kurejesha utawala wa kiraia bado hayajazaa matunda, huku utawala wa kijeshi ukitaka  kipindi cha mpito cha miaka mitatu na Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) ikitoa wito wa kurejeshwa mara moja kwa Bazoum aliyochaguliwa kidemokrasia.

Viongozi wa mapinduzi wa Niger walimshtumu mkuu wa Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa kwa kukwamisha ushiriki wao katika Baraza Kuu la taasisi hiyo, wakisema kuna uwezekano wa kudhoofisha juhudi zozote za kumaliza mzozo katika nchi yao.

Wanajeshi waasi walimpindua rais Mohamed Bazoum Julai 26 na wamemuweka kwenye kizuizi cha nyumbani na familia yake.

Mashauriano ya kurejesha utawala wa kiraia bado hayajazaa matunda, huku utawala wa kijeshi ukitaka kipindi cha mpito cha miaka mitatu na Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) ikitoa wito wa kurejeshwa mara moja kwa Bazoum aliyochaguliwa kidemokrasia.

Mapinduzi hayo pia yamekosolewa vikali na serikali za Magharibi na mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa ambayo inasimamia Mkutano Mkuu wa viongozi wa ulimwengu huko New York wiki hii.

Forum

XS
SM
MD
LG