Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:46

Upinzani Nigeria kupinga matokeo ya uchaguzi mahakama kuu


Wafuasi wa mgombea urais wa chama cha upinzani cha People's Democratic nchini Nigeria, wakihudhuria kampeni ya uchaguzi wa rais katika jiji la Abuja, Nigeria, tarehe 10 Desemba 2022. Picha na AP/Gbemiga Olamikan.
Wafuasi wa mgombea urais wa chama cha upinzani cha People's Democratic nchini Nigeria, wakihudhuria kampeni ya uchaguzi wa rais katika jiji la Abuja, Nigeria, tarehe 10 Desemba 2022. Picha na AP/Gbemiga Olamikan.

Majimbo sita yanayoongozwa na upinzani nchini Nigeria yameiomba mahakama ya juu kutupilia mbali matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, wakisema chombo cha kusimamia uchaguzi kilivunja sheria na kanuni zake wakati wa kuhesabu kura, hati za mahakama zilionyesha.

Mgombea wa chama tawala cha All Progressive Congress (APC) Bola Tinubu alitangazwa mshindi siku ya Jumatano, lakini wapinzani wawili kutoka vyama vikuu vya upinzani walisema matokeo hayo yalikuwa ya udanganyifu na kuapa kuyapinga mahakamani.

Majimbo sita kati ya 36 nchini Nigeria - Adamawa, Akwa Ibom, Bayelsa, Delta, Edo na Sokoto - yalisema kwenye karatasi za mahakama za tarehe 28 mwezi Februari, kuwa tume ya uchaguzi ilishindwa kuwasilisha matokeo kupitia mfumo wa kielektroniki unaokusudiwa kuonyesha uwazi.

Katika ombi lao wameiomba mahakama kutangaza kuwa matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyotangazwa na mwenyekiti wa Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuwa "yalikuwa batili, hayatambuwi, na hayana maana yoyote."

Hakuna majibu ya haraka kuhusiana na suala hilo kutoka serikalini, kampeni la Tinubu, INEC wala mwanasheria Mkuu wa Nigeria, Abubakar Malami, ambaye alitajwa kuwa mhojiwa rasmi kuhusiana na kesi hiyo.

Majimbo hayo sita yanaongozwa na magavana kutoka chama kikuu cha upinzani cha People's Democratic, ambacho mgombea wake Atiku Abubakar alishika nafasi ya pili katika uchaguzi huo, kulingana na matokeo rasmi.

Katika kesi tofauti, mgombea aliyeshika nafasi ya tatu Peter Obi Ijumaa alipewa amri ya mahakama kwa chama chake kupata baadhi ya vifaa vya kutoka INEC, ili kukusanya takwimu kwa ajili ya uwezekano wa kufungua mashtaka. Vifaa hivyo ni pamoja na karatasi na mashine za kupigia kura, amri hiyo ya mahakama ya rufaa ilionyesha.

Obi bado ana wiki tatu za kufungua kesi mahakamani, chini ya sheria ya uchaguzi ya mwaka 2022.

Chanzo cha habari ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG