Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 03:41

Peter Obi adai kushinda uchaguzi Nigeria


Mgombea urais wa Chama cha Labour nchini Nigeria Peter Obi, akizungumza na wafuasi wake wakati wa kampeni za uchaguzi huko Abuja, Nigeria, tarehe 9, Februari 2023. Picha na AP Photo/Emmanuel Osodi.
Mgombea urais wa Chama cha Labour nchini Nigeria Peter Obi, akizungumza na wafuasi wake wakati wa kampeni za uchaguzi huko Abuja, Nigeria, tarehe 9, Februari 2023. Picha na AP Photo/Emmanuel Osodi.

Mgombea urais wa Nigeria Peter Obi alisema Alhamisi kuwa alishinda uchaguzi uliofanyika Jumamosi, na kudai matokeo rasmi yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi yalikuwa ya udanganyifu na kuahidi kutumia vyombo ya sheria kudai ushindi wake.

Mgombea wa chama tawala Bola Tinubu siku ya Jumatano alitangazwa mshindi wa uchaguzi katika taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika.

Kulingana na matokeo rasmi, Tinubu alishinda kwa silimia 37 ya kura, ikilinganishwa na mgombea mkuu wa chama cha upinzani Atiku Abubakar, ambaye alipata asilimia 29, wakati mgombea huyo kutoka chama kidogo cha upinzani ambaye ni maarufu miongoni mwa wapiga kura vijana na wasomi katika meneo ya mijini Obi alipata silimia 25 ya kura.

Vyama vya upinzani vilisema kuwa kura ziliibiwa baada ya teknolojia mpya ambayo tume ya uchaguzi iliahidi kuwa mchakato ulikuwa wa wazi zaidi, badala yake zoezi hilo lilikuwa na utendaji mbaya, uliokosa uaminifu.

Nigeria ina historia ndefu ya vurugu za kisiasa, ingawa hali imezidi kuwa shwari baada ya uchaguzi wenye utata.

Kulikuwepo na changamoto za kisheria kuhusu matokeo ya chaguzi za urais zilizopita nchini Nigeria lakini hakuna iliyofanikiwa.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG