Ushindi unaotarajiwa wa Tinubu unaendelea kukiweka madarakani chama tawala cha All Progressives Congress katika nchi hiyo mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika na yenye watu wengi zaidi duniani. Hata vivyo Tinubu anarithi mlolongo wa matatizo kutoka kwa raisi anayemaliza muda wake.
Huku majimbo manne tu yakiwa yamesalia kutangaza matokeo, Tinubu anaongoza kwa asilimia 34 au kura milioni 7.6 halali zilizo hesabiwa, na kumpa nafasi kubwa ya kutangazwa mshindi Jumanne baada ya uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki.
Vyama vya upinzani vimepinga matokeo hayo ambayo yanatokana na mchakato wenye dosari ambapo ulikumbwa na matatizo mengi ya kiufundi yanayotoakana na kuanzishwa kwa teknologia mpya ya INEC.