Mgombea huyo alikuwa anaongoza katika majimbo 15 kati ya 36 siku ya Jumatatu, lakini vyama vya upinzani vilijiondoa katika mchakato wa kuhesabu kura vikielezea wasiwasi juu ya udanganyifu.
Hesabu ya matokeo ya awali ya tume ya uchaguzi yalionyesha Tinubu, wa chama tawala cha All Progressives Congress (APC), alikuwa mbele kwa takriban kura milioni 4.26, dhidi ya Atiku Abubakar wa chama kikuu cha upinzani cha People's Democratic Party (PDP) kwa takriban kura milioni 3.26.
Mgombea Peter Obi wa chama kidogo cha Labour alikuwa katika nafasi ya tatu na takriban kura milioni 1.77.
Uchaguzi huo umekumbwa na matatizo ya vifaa na teknolojia na yamesababisha kushindwa, katika maeneo mengi, kuweka matokeo moja kwa moja kutoka kila kituo cha kupigia kura hadi kwenye tovuti yake, kama Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) ilivyoahidi kufanya ili kuhakikisha uwazi.