Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:27

ECOWAS yasema Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi Nigeria yashindwa kutimiza ahadi  zake

Watu wakiwa kwenye foleni ya kukusanya kadi zao za wapiga kura kabla ya Uchaguzi wa Urais wa Nigeria Februari 2023 huko Lagos, Nigeria, Jumatano, Januari 11, 2023.
Watu wakiwa kwenye foleni ya kukusanya kadi zao za wapiga kura kabla ya Uchaguzi wa Urais wa Nigeria Februari 2023 huko Lagos, Nigeria, Jumatano, Januari 11, 2023.

Jumuiya ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) ilisema Jumatatu kwamba Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi Nigeria (INEC) ilishindwa katika ahadi  zake kadhaa  ikiwa ni pamoja na kuchelewa na kuwasilisha kimakosa  vifaa kwenye  vituo vya kupigia kura.

Tume ya uchaguzi imekumbwa na matatizo ya vifaa na teknolojia ambavyo vilisababisha kushindwa, katika maeneo mengi, kuweka matokeo moja kwa moja kutoka kila kituo cha kupigia kura hadi kwenye tovuti yake, kama INEC ilivyoahidi kufanya ili kuhakikisha uwazi.

Majimbo kadhaa yaliahirisha upigaji kura kutokana na vurugu za uchaguzi au changamoto za vifaa alisema Mwangalizi Mkuu wa ECOWAS Ernest Koroma.

Kuchelewa kuwasili kwa maafisa wa kupiga kura, vifaa vya kupigia kura, na katika baadhi ya matukio utoaji wa vifaa visivyo sahihi katika vituo vya kupigia kura kote nchini. Kulikuwa na kuahirishwa kwa uchaguzi katika baadhi ya vituo vya kupigia kura katika majimbo ya Lagos, Imo, Bayelsa, Rivers na Enugu kutokana na ghasia za uchaguzi au changamoto za vifaa aliongeza.

Hakuna sharti la kisheria kufanya hivyo, lakini kushindwa kwa tume ya uchaguzi kutimiza ahadi yake kulisababisha matokeo yakusanywe kwa mikono ndani ya vituo vya kuhesabia kura vya kata na serikali za mitaa kama katika uchaguzi uliopita.

XS
SM
MD
LG