Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 19:39

UN na Somalia zaomba bilioni 1.6 kukabiliana na changamoto mbali mbali huko Somalia


Mfanyakazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) alisambaza chakula kwa wanawake wa Somalia Decemba19, 2017. Picha na Zacharias ABUBEKER / AFP
Mfanyakazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) alisambaza chakula kwa wanawake wa Somalia Decemba19, 2017. Picha na Zacharias ABUBEKER / AFP

Umoja wa Mataifa na serikali ya Somalia wameanzisha ombi la dola bilioni 1.6 kwa ajili ya kushughulikia changamoto za kibinadamu nchini Somalia.

Mpango wa utekelezaji wa mahitaji ya kibinadamu ni kutoa misaada ya kuokoa maisha kwa zaidi ya Wasomali milioni tano mwaka huu.

Umoja wa Mataifa umesema mishtuko ya hali ya hewa, migogoro na umaskini uliosambaa pamoja na milipuko ya magonjwa yanaendela kuongeza mahitaji ya kibinadamu katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Ombi hilo limekuja wakati Somalia inajitahidi kukabiliana na ukame wa muda mrefu uliofuatiwa na mvua kubwa na mafuriko mabaya.

“Kwa ujumla hali ya misaada ya kibinadamu nchini Somalia kwa mwaka 2024, Shirika la World Vision linaona mahitaji ya kibanadamu bado yako juu kutokana na kutokea tena kwa mishtuko inayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa na sababu nyingine kama vile migogoro na ukosefu wa usalama” aliseme Suganya Kimbrough, Mkurugenzi wa mpango na maendeleo na uhakiki wa ubora wa shirika la World Vision Somalia.

Lakini idadi ya watu wanaohitaji misaada ya kibinadamu kwa mwaka 2024 imepungua na kufikia milioni 6.9 kutoka milioni 8.2 mwaka 2023, kulingana na rasimu ya karibuni kwa mwaka 2024 ya mpango wa mahitaji na majibu ya kibinadamu ” aliongeza.

Kimbrough amesema fedha kwa ajili ya mfuko wa Umoja wa Mataifa kwa Somalia umefikia dola milioni 56.6, na kuacha pengo kubwa kati ya rasilimali zilizopo na mahitaji.

Ameongeza kuwa pesa nyingi zadi zinakwenda katika masuala ya kuokoa maisha kwa sababu Somalia bado ni tete.

Wasomali takribani milioni tatu wanaishi katika kambi za watu waliopoteza makazi na wengi wao wakitegemea misaada kutoka serikalini na mashirika ya misaada.

Forum

XS
SM
MD
LG