Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 23:24

Ukraine yaendelea kuzithibitishia nchi za Magharibi umuhimu wa kuwapatia silaha za kisasa zaidi


Maafisa wa polisi wanakagua kombora la Russia lililotunguliwa na vikosi vya ulinzi wa anga vya Ukraine huko Mkoa wa Kyiv.
Maafisa wa polisi wanakagua kombora la Russia lililotunguliwa na vikosi vya ulinzi wa anga vya Ukraine huko Mkoa wa Kyiv.

Maafisa wa Jeshi la Ukraine walisema Ijumaa kuwa majeshi ya Russia yameendelea kuishambulia Ukraine, ikisisitiza umuhimu kwa nchi za Magharibi kuwapatia silaha zaidi.

Maafisa wa eneo waliripoti mashambulizi makali kaskazini mwa Ukraine, na katika mikoa ya kaskazini mashariki na mashariki.

Katika hotuba yake ya kila siku kwa taifa Alhamisi, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alitoa shukrani zake kwa kuongezeka idadi ya nchi zinazo ahidi kuwapatia silaha za kisasa, ikiwemo vifaru, wakati huo huo akishinikiza haja ya kuharakisha ahadi ya kufikisha mifumo ya silaha.

Njia pekee ya kusitisha “uchokozi huu wa Russia,” Zelenskyy alisema, “ni kuwa na silaha za kutosha.”

“Taifa hili la kigaidi haliwezi kufahamu kitu kingine chochote,” alisema.

Russia ilianzisha mashambulizi mapya ya makombora katika maeneo kadhaa huko Ukraine Alhamisi, ikiwaua watu 11 na kujeruhi wengine 11, mamlaka zimeripoti.

Idara ya Huduma za Dharura ya Ukraine zimesema mashambulizi hayo yalipiga mikoa 11 nchini humo. Jeshi la anga la Ukraine lilisema Russia ilifyatua makombora 55, huku Ukraine ikifanikiwa kuyatungua karibuni yote. Majengo 35 yameharibiwa katika mashambulizi.

Taarifa katika habari hii imechangiwa na mashirika ya habari ya Reuters na AP.

XS
SM
MD
LG