Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 01:24

Hatua ya kwanza ya kuandaa vikosi viwili venye vifaru vilivyo na nguvu Ukraine njiani


Chansela wa Ujerumani Scholz
Chansela wa Ujerumani Scholz

Berlin itapeleka vifaru 14 aina ya Leopard 2 kwa  Kyiv, ikiwa ni hatua ya kwanza ya kuandaa vikosi viwili venye vifaru vyenye nguvu Ukraine, msemaji wa Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz ametoa taarifa Jumatano.

Taarifa hiyo ilisema vifaru hivyo vitatolewa moja kwa moja kutoka katika ghala ya jeshi la Ujerumani. Pia ilisema kwamba wanajeshi wa Ukraine hivi karibuni wataanza kupatiwa mafunzo nchini Ujerumani, na kuwa Ujerumani itatoa pia utaratibu wa kuvisafirisha na silaha.

Chansela Scholz alitarajiwa kutangaza rasmi uamuzi huo wakati wa kikao cha bunge baadae Jumatano.

Wakati huo huo Marekani na Ujerumani wanaendelea na mipango ya kupeleka vifaru vya kisasa vya kiwango cha juu kuisaidia Ukraine katika vita vyao dhidi ya uvamizi wa Russia ambao umedumu kwa takriban mwaka mmoja.

Uamuzi wa Ujerumani umekuja saa kadhaa kabla ya utawala wa Rais wa Marekani Joe Biden kutarajiwa kutangaza watapeleka vifaru aina ya M1 Abrams kwa Ukraine.

Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Uamuzi huo, kwanza uliripotiwa Jumanne na jarida la The Wall Street, ikiwa ni sehemu ya maelewano ya kidiplomasia na Ujerumani kuhusu msaada wake wa vifaru aina ya Leopard 2.

Vyombo vya habari vya Marekani vinasema utawala unafikiria kupeleka zaidi ya vifaru 30 vya kisasa ili vitumike uwanja mapambano wa Ukraine.

Afisa mmoja wa Marekani ambaye ni mzoefu wa majadilianao hayo ameiambia VOA Jumanne kuwa White House inafanya kazi kukamilisha mpango wa kuipatia Ukraine vifaru wanavyo vihitaji, ingawaje huenda ikachukua muda kabla ya Kyiv kuweza kuvipokea na kuvitumia vifaru hivyo kwenye uwanja wa mapambano.

Afisa huyo, aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa kwa sababu ya unyeti wa mipango hiyo, alisema vifaru hivyo kuna uwezekano vitatolewa kupitia mpango wa msaada wa Pentagon kwa Ukraine maarufu kama Ukraine Security Assistance Initiative (USAI).

Ufadhili unairuhusu Wizara ya Ulinzi kununua silaha na mifumo iwe kutoka kwa watengenezaji wa ulinzi au kutoka kwa vyanzo vingine, kuliko kuchukua moja kwa moja kutoka katika ghala za Marekani.

Katika suala hili, afisa huyo alisema Marekani inaweza kufanya manunuzi ya vifaru vya M1 Abrams kutoka nchi nyingine na kuvikarabati, kabla ya kuvipeleka huko Ukraine.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, ambaye aliahidi kupeleka Ukraine vifaru 14 aina ya Challenger 2, alikubaliana na taarifa kutoka Marekani na Ujerumani katika ujumbe aliyoupachika katika akaunti yake rasmi ya Twitter Jumatano, akisema “ni uamuzi sahihi uliofanywa na washirika wa NATO na marafiki” ambapo “utaimarisha ulinzi wa Ukraine kuweza kupambana na adui.”

“Sote, tunaongeza bidii kuhakikisha Ukraine inashinda vita hii na kupatikana kwa amani ya kudumu,” aliandika Sunak.

Baadhi ya taarifa hii inatokana na ripoti ya mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

XS
SM
MD
LG