Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 13:19

Marekani kutuma vifaru 31 nchini Ukraine


Wanajeshi wa Marekani kwenye kifaru aina M1 Abrahams, wakifanya mazoezi Ujerumani, Juni 2, 2022.
Wanajeshi wa Marekani kwenye kifaru aina M1 Abrahams, wakifanya mazoezi Ujerumani, Juni 2, 2022.

Marekani Jumatano imetangaza kuwa itatuma vifaru 31 aina ya M1 Abrahams nchini Ukraine, vinavyoelezewa na maafisa wa Marekani kuwa “bora zaidi duniani”, vikiwa vinatosha kwa Kyiv kuunda kikosi kamili cha vifaru vya Ukraine.

Uamuzi uliochukuliwa na Washington siku za karibuni, unafuatia wiki kadhaa za mazungumzo na washirika wake wakuu, ikiwemo Ujerumani, na kufungua njia kwa tangazo la Berlin jana Jumatano kwamba itaipa Ukraine vifaru 14 aina ya Leopard 2 na kufungua njia kwa washirika wengine pia kutuma vifaru vilivyotengenezwa na Ujerumani.

“Wakati majira ya msimu wa baada ya baridi yanakaribia, jeshi la Ukraine linafanya kazi kulinda eneo wanaloshikilia na kujiandaa kufanya mashambulizi zaidi ili kuikomboa ardhi yao,” Rais Joe Biden alisema Jumatano, akitangaza uamuzi wa kutuma vifaru nchini Ukraine zaidi ya miezi 11 baada ya wanajeshi wa kwanza wa Russia kuingia Ukraine.

Waukraine wanahitaji kuwa na uwezo wa kukabiliana na mbinu na mikakati ya Russia inayobadilika kwenye uwanja wa vita katika muda wa karibu sana, “Biden aliongeza wakati wa hotuba yake kwenye White House.

XS
SM
MD
LG