Ofisi ya Erdogan, imesema rais alizungumza kwa simu na Putin na kusema kwamba mzungumzo hayo ni vyema yajumuishe haki kwa pande zote.
Kiongozi huyo wa Uturuki, amejaribu kuwa msuluhishi ili kuumaliza mgogoro huo, na pia Uturuki pia ilisadia makubaliano kati ya Russia na Ukraine ili kufanikisha usafirishaji nje wa nafaka. Erdogan alitaraijiwa kuzungumza na rais wa Ukraine baadaye Alhamisi.
Kiongozi mwingine aliyetoa wito wa amani ni Patriarch Kirill, wa kanisa la Orthodox la Russia, ambaye amezitaka pande zote kukubali sitisho la mapigano wakati wa sherehe za Krismas za kanisa la hilo wiki hii.
Afisa mmoja wa Ufaransa amesema Jumatano, raisi wa Ufaransa, Emmanuel Macron amemwambia rais Zelenskyy kuwa Ufaransa itapeleka msaada wa magari ya kivita, aina ambayo imekuwa ikitumiwa na majeshi ya Ufaransa tangu mwaka1980.
“Rais Macron alitaka kuongeza … misaada” kwa Ukraine kwa kuwapatia magari ya kijeshi” msaidizi wa rais Macron ambaye hakutaka jina lake litajwe amewaambia waandishi wa habari baada ya mazungumzo ya simu na kuongeza kuwa “ Ni mara ya kwanza magari ya kijeshi yaliyotengenezwa na magharibi kupewa majeshi ya Ukraine.
Baadhi ya taarifa zilizoko katika habari hii inatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.