Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:10

Waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine auwawa kwenye ajali ya helikopta karibu na Kyiv


Waziri wa mambo ya ndani Denys Monastyrsky, kwenye picha ya awali.June 28, 2022.
Waziri wa mambo ya ndani Denys Monastyrsky, kwenye picha ya awali.June 28, 2022.

Ajali ya helikopta mapema Jumatano nje ya mji mkuu wa Ukraine wa Kyiv, imeua takriban watu 18 akiwemo waziri wa mambo ya ndani Denys Monastyrsky pamoja na maafisa wengine wa ngazi ya juu kutoka katika wizara hiyo.

Ripoti zimesema kwamba ajali hiyo imefanyika karibu na shule ya chekechea, ingawa taarifa kamili za kilichopelekea hazijatolewa. Mkuu wa baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel ametoa rambi rambi zake kwa watu wa Ukraine, wakati akimtaja Monastyrysk kuwa rafiki wa karibu.

Wakati huo huo Marekani pamoja na washirika wengine wa Ukraine wameendelea kutoa misaada ya silaha na mafunzo kwa vikosi vya Ukraine, wakati misaada zaidi ikitarajiwa kutangazwa Ijumaa wakati wa kikao chao kinachoongozwa na Marekani kwenye kituo cha ndege cha jeshi la wanahewa cha Ramstein nchini Ujerumani.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Loyd Austin ataongoza kikao hicho kinachohudhuriwa na darzeni ya mawaziri wenzake pamoja na katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, na waziri wa ulinzi wa Ukraine Olesksii Reznikov.

XS
SM
MD
LG