Russia imeelekeza nguvu zake kwenye kituo kikuu cha mwisho cha idadi ya watu ambacho bado kinashikiliwa na vikosi vya Ukraine katika mkoa wa mashariki wa Luhansk, katika harakati za kufikia moja ya malengo yaliyotajwa ya Rais Vladmir Putin baada ya miezi mitatu ya vita.
Mashambulizi ya mara kwa mara ya makombora yamewaacha wanajeshi wa Ukraine wakilinda magofu huko Sievierodonetsk, lakini kukataa kwao kuondoka kumepunguza kwa kiasi kikubwa kasi ya mashambulizi makubwa ya Russia katika mkoa wa Donbas.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya walitakiwa kukutana leo na kesho kujadili kuhusu vikwazo vipya dhidi ya Russia ikiwemo marufuku ya mafuta.
Kabla ya mkutano, waziri wa uchumi wa Ujerumani Robert Habeck alieleza wasiwasi wake kuhusu umoja wa EU kuanza kusambaratika, rasimu ya yaliyojadiliwa iliyoonekana na ROITA imeashiria kwamba kutakuwa na matokeo madogo katika suala la maamuzi mapya.