Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 04:46

Jeshi la Russia lasema limeuteka mji wa Lyman


FILE - Watu wakiwa ndani ya basi wakati wakiondolewa katika eneo karibu na mji wa Lyman, Ukraine, Jumatano May 11, 2022.
FILE - Watu wakiwa ndani ya basi wakati wakiondolewa katika eneo karibu na mji wa Lyman, Ukraine, Jumatano May 11, 2022.

Jeshi la Russia linasema limeuteka mji wa Lyman ulioko mashariki mwa Ukraine, kituo kikuu cha treni katika mkoa wa Donetsk.

Kutekwa huko kunaweza kuashiria kubadilika kwa kasi ya vita vya Ukraine.

“Kufuatia hatua za pamoja za vikosi vya wanamgambo wa Jamhuri ya watu wa Donetsk na majeshi ya Russia, mji wa Krasny Liman umekombolewa kikamilifu kutoka kwa wazalendo wa Ukraine,” wizara ya ulinzi imesema katika taarifa yake, ikitumia jina la Kirusi kuutaja mji wa Lyman.

Siku ya Jumamosi, Russia pia ilisema kuwa imefanikiwa kujaribu makombora ya hypersonic katika eneo la Arctic. Wizara ya Ulinzi imesema makombora ya Zircon hypersonic yaliruka umbali wa kilomita 1,000 na kufanikiwa kupiga shabaha iliyowekwa huko Arctic.

Jaribio la kombora la (Zircon) hypersonic cruise missile July 19, 2019. Russian Defence Ministry/Handout via REUTERS ATTENTION EDITORS - THIS IMAGE WA
Jaribio la kombora la (Zircon) hypersonic cruise missile July 19, 2019. Russian Defence Ministry/Handout via REUTERS ATTENTION EDITORS - THIS IMAGE WA

Kuchukua udhibiti wa Lyman unaiweka nafasi ya Russia kuanza awamu ya pili ya mashambulizi katika mkoa wa Donbas.

Mji huo uko kilomita 40 magharibi mwa Sievierodonetsk mji mkubwa zaidi wa Donbas ambao unaendelea kushikiliwa na majeshi ya Ukraine.

Sievierodonetsk, inayolengwa hasa katika mashambulizi yanayofanywa na Moscow, uko katika mashambulizi mazito. Gavana wa mkoa Luhansk , ambao pamoja na Donetsk unaunda Donbas, alisema Ijumaa kuwa vikosi vya Russia vimeingia Sievierodonetsk.

“Iwapo Russia itafanikiwa kuyachukua maeneo haya, upo uwezekano mkubwa Kremlin kuangalia hili kama ni mafanikio makubwa ya kisiasa na kuonyeshwa kwa watu Russia kama kilichohalalisha uvamizi,” wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Jumamosi.

Mkoa wa mashariki wa Donbas ni eneo kuu la viwanda la Ukraine na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ameishutumu Moscow kwa kutekeleza “mauaji ya kimbari” huko

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy

Katika hotuba yake ya usiku Ijumaa, Zelenskyy amesema Ukraine itajihami “kwa kadri ya uwezo wa kijeshi wa hivi sasa waliokuwa nao.”

Alitoa tamko la kukaidi hatua ya mashambulizi ya Russia katika upande wa mashariki ya Ukraine: “Iwapo wavamizi hawa wanafikiri kuwa Lyman au Sievierodonetsk zitakuwa zao, hawako sahihi, Donbas itabakia kuwa ya Ukraine.

XS
SM
MD
LG