Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 17:40

Vikwazo vilivyochukuliwa dhidi ya Russia vyaathiri nchi zisizohusika na mzozo wa Ukraine, anasema Ramaphosa


Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, wakiendesha mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Pretoria, May 24, 2022. Picha ya AFP
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, wakiendesha mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Pretoria, May 24, 2022. Picha ya AFP

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Jumanne amesema nchi zisizohusika na mzozo wa Ukraine zinaathirika kutokana na vikwazo vilivyochukuliwa dhidi ya Russia, na ametoa wito wa mazungumzo wakati Umoja wa Afrika unaandaa tume ya kuendeleza mazungumzo kati ya Moscow na Kyiv.

Ramaphosa alisema hayo wakati Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa ziarani nchini Afrika Kusini, ziara yake ya mwisho barani Afrika ambayo kwa sehemu moja ilikuwa na lengo la kutafuta uungwaji mkono wa kidiplomasia kwa Ukraine.

Afrika Kusini ina uhusiano wa karibu wa kihistoria na Moscow kutokana na uungwanji mkono wa umoja wa zamani wa Soviet katika vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.

Ilijizuia kupigia kura azimio la Umoja wa mataifa ambalo lililaani uvamizi wa Ukraine, na haikuitikia wito wa kuilaani Russia kwa uvamizi huo.

Umoja wa Ulaya uliendelea kuchukua vikwazo vikali vya kiuchumi kuiadhibu Moscow kwa operesheni zake za kijeshi nchini Ukraine, mkakati ambao Ramaphosa amesema unasababisha madhara mabaya.

“Hata nchi hizo ambazo zinatizama kwa mbali au hazihusiki na mzozo zitaathirika pia kutokana na vikwazo vilivyochukuliwa dhidi ya Russia,” amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Pretoria.

Afrika, ambayo tayari mamilioni ya raia wake wamejikuta kwenye umaskini mkali kutokana na janga la corona, imekumbwa vibaya na gharama za juu za chakula zilizosababishwa kwa sehemu moja na uhaba wa chakula unaohusiana na vita vya Ukraine.

Russia na Ukraine zinachangia karibu theluthi moja ya ngano duniani, na theluthi mbili ya mafuta ya alizeti yanayouzwa nje kwa kupikia.

XS
SM
MD
LG