Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 20:27

Zelenskyy: Ukraine inahitaji silaha nyingi zaidi kupambana na Russia


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy akitembelea eneo ambalo majeshi ya Ukraine yanapambana na majeshi ya Russia kufuatia Russia kuivamia Ukraine, katika mkoa wa Kharkiv, Ukraine May 29, 2022. (Ukrainian Presidential Press Service/Handout via Reuters)
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy akitembelea eneo ambalo majeshi ya Ukraine yanapambana na majeshi ya Russia kufuatia Russia kuivamia Ukraine, katika mkoa wa Kharkiv, Ukraine May 29, 2022. (Ukrainian Presidential Press Service/Handout via Reuters)

“Tunafanya kazi kila siku kuimarisha ulinzi wetu. Hii kimsingi ni kupata silaha,” alisema.

Katika hotuba yake ya kila Jumamosi, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amrejea kusisitiza haja ya nchi yake kupatiwa silaha.

“Tunafanya kazi kila siku kuimarisha ulinzi wetu. Hii kimsingi ni kupata silaha,” alisema.

“Bila shaka, kwa kiwango kikubwa inategemea na washirika wetu. Kwa utayari wao wakuipatia Ukraine kila kilicho muhimu kulinda uhuru wetu.”

Gazeti la New York Times linaripoti kwamba Ukraine “imepatiwa silaha na Denmark makombora ya Harpoon ya kujilinda na mashambulizi ya manowari za kivita,” wakati Ukraine ikihangaika kuizuia Russia kuchukua kikamilifu udhibiti wa mkoa wa Donbas ulioko mashariki mwa nchi hiyo.

Majeshi ya Russia yanasema yameuchukua mji wa mashariki mwa Ukraine wa Lyman, kituo kikuu cha treni katika mkoa wa Donetsk. Kutekwa kwa mji huo kunaashiria mabadiliko ya kasi ya vita huko Ukraine.

“Kufuatia hatua za pamoja za vikosi vya wanamgambo wa Jamhuri ya watu wa Donetsk na majeshi ya Russia, mji wa Krasny Liman umekombolewa kikamilifu kutoka kwa wazalendo wa Ukraine,” wizara ya ulinzi imesema katika taarifa yake, ikitumia jina la Kirusi kuutaja mji wa Lyman.

Siku ya Jumamosi, Russia pia ilisema kuwa imefanikiwa kujaribu makombora ya hypersonic katika eneo la Arctic. Wizara ya Ulinzi imesema makombora ya Zircon hypersonic yaliruka umbali wa kilomita 1,000 na kufanikiwa kupiga shabaha iliyowekwa huko Arctic.

Kuchukua udhibiti wa Lyman unaiweka nafasi ya Russia kuanza awamu ya pili ya mashambulizi katika mkoa wa Donbas.

Mji huo uko kilomita 40 magharibi mwa Sievierodonetsk mji mkubwa zaidi wa Donbas ambao unaendelea kushikiliwa na majeshi ya Ukraine.

Sievierodonetsk, inayolengwa hasa katika mashambulizi yanayofanywa na Moscow, uko katika mashambulizi mazito. Gavana wa mkoa Luhansk , ambao pamoja na Donetsk unaunda Donbas, alisema Ijumaa kuwa vikosi vya Russia vimeingia Sievierodonetsk.

XS
SM
MD
LG