Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:48

Ugiriki yawaokoa wahamiaji zaidi ya 100 nje ya kisiwa cha Mykonos


FILE - Wahamiaji wakiwa katika boti ya plastiki wakikaribiwa na walinzi wa pwani ya Ugiriki katika bandari ya Thermi, wakiwa wanavuka sehemu ya Bahari ya Aegean kutokea Uturuki wakielekea visiwa vya Lesbos, Ugiriki, March 1, 2020.
FILE - Wahamiaji wakiwa katika boti ya plastiki wakikaribiwa na walinzi wa pwani ya Ugiriki katika bandari ya Thermi, wakiwa wanavuka sehemu ya Bahari ya Aegean kutokea Uturuki wakielekea visiwa vya Lesbos, Ugiriki, March 1, 2020.

Zaidi ya wahamiaji 100 wameokolewa mapema Jumapili nje ya kisiwa cha Mykonos katika Bahari ya Aegean na wengine wanne hawajulikani walipo, mlinzi wa pwani ya Ugiriki amesema.

Polisi wa bandari walijibu taarifa ya hatari walituma boti tatu na boti ya kuvutwa kusaidia chombo kilichokuwa hatarini kilichokuwa kinatokea Uturuki, walinzi wa pwani waliliambia shirika la habari la AFP.

Imeelezwa kuwa watu 108 waliokolewa na wengine wanne hawajulikani waliko.

Idadi ya wote waliokuwa katika chombo haijathibitishwa kutokana na taarifa zinazokinzana zilizowasilishwa na waokoaji hao, imeongeza kusema.

Waziri wa Uhamiaji Notis Mitarachi hapo awali alituma ujumbe wa Twitter ukisema wahamiaji wanane walikuwa hawajulikani waliko na 104 walikuwa wameokolewa.

Pia aliitaka Uturuki kufanya utaratibu mzuri zaidi ili kulinda maisha ya binadamu na kukomesha mtandao wa wasafirishaji haramu.

Mwezi May, Mamlaka nchini Ugiriki zilisema wamezuia wahamiaji 600 kuvuka Bahari ya Aegean kuja katika eneo la majini la himaya yao wakitokea nchi jirani ya Uturuki katika siku moja, ikiwa ni jaribio kubwa la wahamiaji hao mwaka huu.

Vyanzo vya Wizara ya Uhamiaji vilikuwa vimesema wimbi la wahamiaji kuingia visiwa vya Ugiriki katika miezi minne ya mwanzo wa mwaka 2022 lilikuwa juu kwa takriban asilimia 30 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2021.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG