Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:38

Boti iliyokuwa imebeba wahamiaji 100 yazama nje ya pwani ya Tunisia


Sfax Tunisia
Sfax Tunisia

Watu 76 wameripotiwa hawajulikani walipo baada ya boti iliyokuwa imewabeba watu 100 kuzama karibu na mji kusini mashariki mwa mji wa Sfax nchini Tunisia.

Watu 76 wameripotiwa hawajulikani walipo baada ya boti iliyokuwa imewabeba watu 100 kuzama karibu na mji kusini mashariki mwa mji wa Sfax nchini Tunisia.

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM nchini Tunisia limeandika katika mtandao wake wa twitter kwamba mwili mmoja umepatikana hadi sasa na wengine 30 waliokolewa na walinzi wa pwani wa Tunisia.

Kwa mujibu wa mtandao binafsi wa habari wa Tunisia wa Kapitalist boti hiyo iliyokuwa imejaa watu ilikuwa ikisafiri kutoka ufukwe wa Zuwara nchini Libya karibu na mpaka wa Tunisia.

Habari hizo zimekuja siku mbili tu baada ya boti nyingine mbili kuzama kwenye pwani katika jimbo la SFAX.

Katika moja ya matukio, raia wanane wa Tunisia kutoka mji wa mwambao wa kati wa Monastir hawajulikani walipo, kwa mujibu wa radio ya taifa ya Shems FM.

Takriban wahamiaji wengine wanne wamekufa na 10 wameripotiwa hawajulikani walipo katika tukio jingine kufuatia boti iliyozama ikiwa na wahamiaji 58.

Tunisia ni moja ya njia kuu afrika kwa ajili ya wahamiaji wanaojaribu kuingia Ulaya. Wengi wanatokea katika nchi Afrika chini ya jangwa la Sahara.

XS
SM
MD
LG