Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:39

Polisi wa Ufaransa wamevunja kambi ya wahamiaji kutoka Iraq


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron

Polisi nchini Ufaransa wamevunja kambi ya mamia ya wahamiaji karibu na mji wa Dunkirk, baada ya mtu mmoja kuuawa na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia makabiliao kati ya wahamiaji na watu wanaofanya biashara ya magendo.

Karibu watu 500, wengi wao wakiwa wakurd kutoka Iraq, wamekuwa wakiishi katika kambi hiyo yeye nyumba za mbao iliyo karibu a sehemu ambapo boti zinazotoka Uingereza hadi Ulaya hupakia.

Mhamiaji mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi jumatatu usiku na mwingine kujeruhiwa.

Watu wawili walikuwa wamepigwa risasi na kujeruhiwa siku mbili kabla, mmoja wao alijeruhiwa vibaya.

XS
SM
MD
LG