Serikali ya Uingereza ambayo mwezi uliopita ilipanga kuwapeleka wanaotafuta hifadhi katika taifa hilo la Afrika mashariki la Rwanda, imesema kwamba ilitarajia wanasheria wanao kuwakilisha baadhi yao kuwasilisha madai yatakayo wazuia kuondolewa nchini humo, ambapo ndege ya kwanza inatarajiwa kuondoka katika kipindi cha miezi michache ijayo.
Hii ni hatua ya kwanza ya mchakato, na tunafahamu itachukuwa muda kutokana na kwamba baadhi yao watataka kuuvuruga mpango huo na kuchelewesha watu hao kupelekwa Rwanda, alisema waziri wa mambo ya ndani, Priti Patel katika taarifa.