Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:33

Wahamiaji 44 wafa maji katika pwani ya Western Sahara


 Wahamiaji wanaonekana ndani ya boat yao wakiwasili katika bandari ya Christianos kwenye ksiiwa cha Spain cha Canary, August 1, 2006. Picha ya AP
Wahamiaji wanaonekana ndani ya boat yao wakiwasili katika bandari ya Christianos kwenye ksiiwa cha Spain cha Canary, August 1, 2006. Picha ya AP

Wahamiaji 44 wamekufa maji Jumapili wakati boti yao ilipozama katika pwani ya Western Sahara, shirika linalosaidia wahamiaji Caminando Fronteras limesema.

Wengine 12 wamenusurika kwenye ajali hiyo mbaya, ambayo ilitokea wakati boti hiyo ilipozama kwenye ufukwe wa Cap Boujdour, afisa wa shirika hilo Helena Maleno ameandika kwenye Twitter.

Maleno ameandika kwamba manusura wamekamatwa.

Miili ya waathirika saba ilipelekwa ufukweni lakini wengine hawakuweza kupatikana, Maleno ameongeza.

Viongozi wa Morocco ambao wanadai eneo hilo lenye utata la Western Sahara kuwa ni sehemu ya taifa hilo la kifalme la Afrika magharibi, hawakuthibitisha mara moja ajali hiyo.

Haikufahamika wazi wapi boti hiyo ilikuwa inaelekea, lakini wahamiaji wanaosafiri kutoka eneo hilo hujaribu kufika kwenye visiwa vya Canary nchini Spain.

Morocco ni kituo muhimu kinachotumiwa na wahamiaji kama njia ya kusafiri kuelekea Ulaya ili kutafuta maisha bora.

XS
SM
MD
LG