Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:31

Wahamiaji waliokusudia kuingia Marekani wamejipata Cuba


Wahamiaji kutoka Haiti na Amerika ya kati kwenye mpaka wa Tijuana, Mexico
Wahamiaji kutoka Haiti na Amerika ya kati kwenye mpaka wa Tijuana, Mexico

Boti lililokuwa limebebea wahamiaji 800 kutoka Haiti wakielekea Marekani, limelazimika kutua kwenye pwani ya kati ya Cuba Cuba, katika kile kinaonekana kama kundi kubwa zaidi la wahamiaji kuwahi kuondoka Haiti inayokumbana na migogoro kadhaa.

Shirika la msalaba mwekundu katika mkoa wa Villa Clara, limesema kwamba wahamiaji 842 wamepewa makao ya m da katika kambi ya watalii.

Wahamiaji hao waliwasili Jumanne, katika mji wa Villa Blanca, kilomita 300 mashariki mwa Havana. Miongoni mwao ni watoto 70 na wanawake 97.

Wamesema kwamba waliitisha msaada baada ya kuachwa baharini na nahodha wa boti hilo.

Walinzi wa pwani ya Marekani, pamoja na walinzi wan chi zingine wameripoti kukamata boti kadhaa zilizokuwa zimebeba zaidi ya wahamiaji 100 wa Haiti, katika miezi ya hivi karibuni.

XS
SM
MD
LG