Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 14:37

Ndege ya kwanza ya wakimbizi kutoka Uingereza hadi Rwanda kuondoka Jumanne


Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Priti Patel na waziri wa mambo ya kigeni wa Rwanda Vincent Biruta
Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Priti Patel na waziri wa mambo ya kigeni wa Rwanda Vincent Biruta

Safari ya kwanza ya ndege ya Uingereza iliyopangwa kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda ilikuwa iondoke Jumanne, huku serikali ikionya kwamba yeyote atakayakwepa dakika za mwisho kwa kutumia changamoto za kisheria atasafirishwa baadaye.

Uingereza imefikia makubaliano ya paundi milioni 120 (dola milioni 148) na Rwanda kutuma baadhi ya wahamiaji, ambao walivuka kinyume cha sheria kupitia eneo dogo la bahari kwa kutumia boti kutoka Ulaya, ili kuishi katika nchi hiyo ya Afrika isiyo na bandari.

Mpango huo umewatia hofu wapinzani wa kisiasa, mashirika ya misaada na viongozi wa makanisa wanaosema kuwa ni kinyume cha ubinadamu. Mkuu wa wakimbizi wa Umoja wa Mataifa aliliita ni janga, uongozi mzima wa Kanisa la Uingereza ulishutumu kama sera zisizo na maadili zinazoaibisha Uingereza.

Serikali inasema mkakati wa kuwafurusha unahitajika ili kukomesha mtiririko wa wahamiaji wanaohatarisha maisha yao katika vivuko vya baharini na kuvunja mitandao ya magendo ya watu.

XS
SM
MD
LG