Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 20:29

Uganda yahamisha haki za usambazaji petroli kutoka Kenya na kuipa kampuni ya Vitol


Waendesha bodaboda wakisubiri kujaza mafuta katika kituo cha mafuta huko Kampala Januari 19, 2022. Picha na Badru KATUMBA/AFP.
Waendesha bodaboda wakisubiri kujaza mafuta katika kituo cha mafuta huko Kampala Januari 19, 2022. Picha na Badru KATUMBA/AFP.

Uganda inapanga kukabidhi haki za kipekee za usambazaji wa bidhaa zote za petroli kwa kampuni ya biashara ya nishati duniani ya Vitol na kuachana na mfumo wa vyanzo vya bidhaa za mafuta unaopitia nchi jirani ya Kenya, waziri wa nishati wa Uganda amesema.

Makampuni ya mafuta katika taifa hilo la Afrika Mashariki lisilo na bandari hununua bidhaa zao kupitia makampuni husika nchini Kenya ambayo yanaagiza bidhaa kwa niaba yao kupitia bandari ya Mombasa.

Mfumo huo, ambao unahusisha takriban asilimia 90 ya mafuta yanayoagizwa na Uganda, unaweka wazi usumbufu wa usambazaji na bei kwenye vituo vya petroli, Waziri wa Nishati Ruth Nankabirwa alisema katika taarifa yake.

"UNOC na Vitol Bahrain E.C. wamekuwa wakifanya majadiliano ya mkataba wa miaka mitano, na Mshirika (Vitol) atakuwa akifadhili biashara kwa kutoa mtaji wa kufanya kazi," alisema Jumanne jioni.

Kulingana na takwimu za benki kuu, Uganda iliagiza bidhaa za petroli kutoka nje zenye thamani ya dola bilioni 1.6 mwaka 2022.

Baraza la mawaziri limeidhinisha mabadiliko ya sheria ya petroli ambayo itairuhusu kampuni yaVitol kuwa msambazaji pekee kwa Kampuni ya Taifa ya Mafuta Uganda inayomilikiwa na serikali (UNOC), alisema waziri huyo.

UNOC nayo itauza bidhaa hizo kwenye vituo vya uuzaji wa mafuta.

Ili kuhakikisha usalama wa usambazaji kwa Uganda, Vitol na UNOC zitaanzisha "hifadhi ya akiba" nchini Uganda na nchi jirani ya Tanzania, Nankabirwa alisema.

Dereva wa pikipiki akisukuma pikipiki yake kutoka kwenye kituo cha mafuta ambacho kiliishiwa mafuta huko Kampala Uganda Januari 18, 2022. Picha na Badru KATUMBA/AFP.
Dereva wa pikipiki akisukuma pikipiki yake kutoka kwenye kituo cha mafuta ambacho kiliishiwa mafuta huko Kampala Uganda Januari 18, 2022. Picha na Badru KATUMBA/AFP.

Kutumia waagizaji wa Kenya "kumeweka wazi udhaifu wa Uganda wa mara kwa mara katika usambazaji, ambapo makampuni yanayouza rejareja ya Uganda yamekuwa yakitumika wakati wa usumbufu wa usambazaji," kitendo ambacho kinaathiri bei za rejareja, Nankabirwa alisema.

Mwezi Machi, Kenya iliingia mkataba na Saudi Aramco, Kampuni ya Kitaifa ya Mafuta ya Abu Dhabi na kampuni ya mafuta ya Taifa ya Emirates, ilibadili kutoka mfumo wa wazi wa zabuni ambao makampuni ya ndani ya Kenya hutoa zabuni ya uagizaji mafuta kutoka nje kila mwezi.

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli ya Kenya haikuwa na maoni ya haraka kuhusu mabadiliko yanayopendekezwa na Uganda.

Chanzo Cha habari hii ni sirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG