Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 01:46

Rais Yoweri Museveni aapa vikosi vya Uganda vitawasaka waliohusika na mauaji ya watalii


Rais wa Uganda Yoweri Museveni alipokuwa jijini Nairobi, Kenya Februari 25. 11, 2020.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni alipokuwa jijini Nairobi, Kenya Februari 25. 11, 2020.

Rais Yoweri Museveni aliapa kwamba vikosi vya Uganda vitawasaka waliohusika na vifo vya muongoza watalii na watalii wawili wa kigeni waliokuwa wakienda fungate katika mbuga ya wanyama.

Rais Yoweri Museveni aliapa siku ya Jumatano kwamba vikosi vya Uganda vitawasaka waliohusika na vifo vya muongoza watalii na watalii wawili wa kigeni waliokuwa wakienda fungate katika mbuga ya wanyama.

Mamlaka za Uganda zimeshutumu kundi la Allied Democratic Forces (ADF) kwa kuwaua wanandoa hao, raia wa Afrika Kusini na raia wa Uingereza, na muongoza watalii wa Uganda siku ya Jumanne jioni karibu na Mbuga ya Kitaifa ya Queen Elizabeth.

Kundi la ADF, ambalo lilianza kama la uasi nchini Uganda lakini limeweka makao yake katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tangu mwishoni mwa miaka ya 1990, liliahidi utiifu kwa Islamic State miaka minne iliyopita.

Baada ya kufanya kazi nchini Congo kwa miaka mingi, imeongeza mashambulizi ndani ya Uganda katika miezi ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na uvamizi wa mwezi Juni katika shule ya sekondari ambayo iliua zaidi ya watu 40.

Forum

XS
SM
MD
LG