Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 23:00

Marekani yatoa tahadhari ya kufanya biashara na Uganda


Wizara za Marekani za mambo ya nje, kazi, afya na huduma za kibinadamu, biashara, na shirika la maendeleo la kimataifa la Marekani, Jumatatu zimetoa tahadhari ya kibiashara dhidi ya Uganda.

Tahadhari hiyo inazifahamisha biashara na watu binafsi wa Marekani, wakiwemo watoa huduma za afya, maafisa wa taasisi za kitaaluma na wawekezaji, kuhusu athari zinazoweza kuwakabili ikiwa watafanya au kutafakari kufanya biashara nchini Uganda.

Biashara, mashirika na watu binafsi wanapaswa kufahamu athari zinazoweza kutokea za kifedha na sifa zinazotokana na ufisadi uliokithiri, uliofafanuliwa kwa undani zaidi katika taarifa ya hali ya uwekezaji ya 2023.

Yale yaliyoelezwwa na ripoti yanajumuisha unyanyasaji dhidi ya wanaharakati wa haki za binadamu, wanahabari, wafanyikazi wa afya, watu wa makundi ya walio wachache, watu wa kundi la LGBTQI+, na wapinzani wa kisiasa walioelezwa katika ripoti ya nchi ya 2022 kuhusu matendo ya haki za Kibinadamu nchini Uganda.

Forum

XS
SM
MD
LG